Hair Care: Washing Tips
Hits: 464

1.       Osha nywele angalau mara 1 moja kwa wiki. Mafuta na uchafu huziba vishimo vya ngozi ya kichwa na kuzuia mzunguko wa damu ulio muhimu katika kukua kwa nywele.

 

 1. Tumia shampoo zilizotengenezwa na vitu asilia. Kemikali zilizomo katika shampoo nyingi huwa ni kali na hukausha nywele zako.
 2. Kama nywele zako si chafu sana zioshe kwa kutumia conditioner badala ya shampoo. Conditioner husafisha kama shampoo lakini ina kemikali chache zaidi.
 3. Nywele za Kiafrika zina asili ya ukavu na hivyo matumizi ya shampoo kali huchangia ukavu huo. Jaribu kuosha nywele zako na conditioner zaidi kuliko shampoo.
 4. Paka mafuta asili kama ya nazi au mzeituni katika nywele angalau nusu saa kabla ya kuosha ili kusaidia kulinda nywele na ukali wa shampoo.
 5. Kabla ya kuosha nywele hakikisha kuwa umechana nywele zako na kuondoa mafundo yeyote yanayoweza kusababisha kukatika kwa nywele.
 6. Unapoosha nywele zako, paka shampoo katika ngozi na sio kwenye nywele. Uchafu mwingi huwa kwenye ngozi na sio katika shina la nywele.
 7. Povu moja la shampoo linatosha kusafisha nywele zako. Matumizi ya shampoo yaliyopitiliza huchangia kufanya nywele kuwa kavu.
 8. Sugua ngozi ya kichwa taratibu kwa kutumia vidole vyako na sio kucha wakati wa kuosha nywele zako.
 9. Unapoweka conditioner baada ya kuosha nywele na shampoo, hakikisha hupaki conditioner katika ngozi bali katika shina na ncha za nywele kuepuka ngozi kavu.
 10. Tumia maji ya vuguvugu kuosha nywele zako. Maji ya moto yatafanya nywele zako kuwa kavu na ya baridi hayayeyushi mafuta na taka ng’ang’anizi kwenye nywele.
 11. Tumia leave-in conditioner kila uoshapo nywele zako. Hii hurutubisha nywele, kuhifadhi unyevu kwa kufunga shina la nywele ambalo hufunguka wakati wa kuosha.
 12. Unapochana nywele zako zikiwa na unyevu wa maji wakati wa kuosha, tumia chanuo lenye meno makubwa kuzuia kukatika kwa nywele.
 13. Usifute nywele zako na taulo na usipende kutumia moto kukausha nywele. Nywele zetu zinahitaji unyevu wa kutosha na taulo hupitiliza kukausha.
 14. Kukausha nywele zako, kamua maji yaliyozidi katika nywele halafu soma kitabu au pitia blogu ya Kidoti kuruhusu nywele zako kukauka na hewa ya kawaida.