Facial Tips: Skin Treatment
Hits: 311

1.       Scrub uso wako angalau mara 1 na si zaidi ya mara 3 kwa wiki. Kama sabuni, kuwa mwangalifu unaponunua scrub zilizotengenezwa kiwandani. 

 1. Unaposugua uso wako na scrub usitumie nguvu. Sugua taratibu kisha suuza uso wako na maji ya baridi.
 2. Osha uso kisha chukua magadi kidogo, changanya na matone ya maji halafu paka usoni. Acha kwa dakika 5 kisha sugua taratibu. Huondoa ngozi ya juu iliyokufa.
 3. Unapofanya scrub hakikisha unakwepa ngozi inayozunguka macho na pembeni mwa mdomo. Ngozi hii ni laini na hulegea kirahisi ikisuguliwa kwa nguvu.
 4. Unapoosha uso wako au kufanya scrub, vishimo vya ngozi yako hufunguka. Ili kufunga vishimo vya ngozi tumia toner kila mara.
 5. Toner asilia na rafiki kwa mfuko wako ni pamoja na maji ya waridi, juisi ya limao na maji ya tango.
 6. Ununuapo toner ya dukani hakikisha haina “alcohol” kama moja ya viungo vyake. Alcohol ni kali, huchangia kukausha ngozi na kupelekea maambukizi ya ngozi.
 7. Kuondoa makovu na madoa, paka mchanganyiko wa asali na juisi ya limao usoni mara moja kwa siku, acha kwa dakika 20 kisha suuza na maji baridi.
 8. Kuzuia kushamiri kwa uvimbe wa chunusi unaonza usoni kwako, chukua barafu na sugua eneo lililoathirika kwa dakika 15. Fanya hivi angalau mara tatu kwa siku.
 9. Paka mask angalau mara moja kwa wiki ili kuipa ngozi yako virutubisho muhimu.
 10. Mask ya karoti na asali: Karoti inajulikana kwa kuwa na vitamini A na C pia potasiamu na asali huwa ina sukari, enzymes, madini, vitamini na amino asidi.
 11. Mask ya asali na juisi ya limao husaidia kusafisha ngozi,  kuondoa makovu na kungarisha ngozi yako kwa kuhifadhi unyevu asilia wa ngozi.
 12. Kukuza kope na nyusi paka mafuta kwa kuzamisha ncha ya kijiti cha kusafishia sikio katika mafuta ya mbarika au mrozi kisha paka kila siku kabla ya kulala.
 13. Fanya facial angalau mara moja kwa mwezi. Hakikisha kuwa unafanyiwa facial itakayokidhi mahitaji ya ngozi yako kwa wakati huo mfano kusafisha.
 14.  Paka sunscreen kwenye ngozi ya uso wako baada ya facial kwani ngozi inayobakia huwa rahisi kudhurika na mionzi mikali ya jua.