Jina La Kidoti

Jina la Kidoti limetokana na alama ama kipele cheusi kilichopo chini ya pua yangu ama juu ya mdomo wangu kutokana na vile mwenyewe utakavyamua kutazama:) lilianza kama jina la utani, watu wengi wakilitumia ku-identify na mimi lakini kwa sasa nimegeuza ule utani, ile alama kuwa biashara na alama ya viwango vya kimapinduzi ninavyotaka kufanya pamoja na wenzangu katika tasnia ya urembo na mitindo hapa nchini Tanzania naa Afrika kwa ujumla wake.

Kidoti ilianza kujitambulisha kupitia nguo zake ambazo zilikuwa ni custom made, one-off pieces na siyo kwenye collection. Lengo likiwa ni kuwazoesha watu na jina Kidoti lakini pia watu waanze kuzoea mambo tofauti katika tasinia yetu hii ya mitindo na urembo.